1 Desemba 2025 - 12:41
Marekani na Israel wanaandaa / Wanatengeneza simulizi (riwaya) mpya ili kuongeza shinikizo dhidi ya Hezbollah na Lebanon

Israel, kwa msaada wa Marekani, inajaribu kutengeneza mazingira ya kuanzisha vita na kuongeza mashinikizo dhidi ya Lebanon, kwa kutishia kulazimisha Hezbollah ivuliwe silaha kufikia mwisho wa mwaka.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa utawala wa Kizayuni, kwa msaada wa Marekani, unajenga simulizi mpya inayodai kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano na Lebanon yameshindikana, na simulizi hilo linatumika kama utangulizi wa kuongeza shinikizo dhidi ya Hezbollah na serikali ya Lebanon.

Gazeti la Al-Akhbar la Lebanon liliandika kuwa: Israel katika propaganda zake inadai kuwa Hezbollah inaendelea kujenga upya uwezo wake wa kijeshi; madai haya yalijitokeza sambamba na mauaji ya kishahidi ya “Haitham Tabatabai”, kamanda wa kijeshi wa Hezbollah, pamoja na wenzake.

Udhibiti wa kijeshi wa habari wa utawala wa Kizayuni umezuia kusikika wazi kauli ya Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hezbollah, aliyesisitiza kuwa: “Harakati ina haki ya kujibu, na wakati wa kujibu ni uamuzi wetu wenyewe.”

Vyombo vya habari na duru zinazohusishwa na Israel vimeonya kuwa majibu yoyote kutoka kwa Hezbollah yatafuatiwa na hatua kali zaidi kutoka Israel, sawa na shinikizo la kidiplomasia la mwaka uliopita lililolenga kuizuia Hezbollah kujibu mauaji ya viongozi wake.

Ziara ya Badr Abdelatty, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, huko Beirut pia ilikamilika bila mafanikio ya maana; vyanzo vya kuaminika vimebainisha kuwa hakukuwa na mkutano wowote na Hezbollah, na kwamba suala la mgogoro na Israel bado linafuatiliwa kupitia kitengo cha Ujasusi cha Misri.

Katika wiki za karibuni, Marekani na Israel zimekuwa zikiunda simulizi la pamoja linalodai kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano yameshindwa, na zinataka Lebanon ianze mazungumzo ya moja kwa moja na Israel. Lengo la mazungumzo haya, kama wanavyodai, ni kuvuliwa silaha kwa Hezbollah kabla ya mwisho wa mwaka.

Jenerali mmoja wa Israel amesisitiza kuwa makubaliano ya usalama si chochote zaidi ya kununua muda, na kwamba mkakati wa mwisho unapaswa kuwa kubadilisha mazingira yote ya eneo hilo na kuondoa kabisa uwezo wa Hezbollah.

Israel kupitia kile inachoita “vita baina ya vita”—ikiwa ni pamoja na mauaji ya kulenga, kuharibu maghala, kushambulia miundombinu na kuendesha vita vya kisaikolojia—inalenga kuidhoofisha Hezbollah hatua kwa hatua na kuisukuma Lebanon katika hali ambayo haitakuwa na uwezo wa kubeba gharama ya kuwepo kwa Hezbollah kama jeshi linaloendesha shughuli sambamba na serikali.

Mkakati huo pia unajumuisha:

  • shinikizo la kiuchumi, kwa kukata njia za kifedha kutoka Iran,

  • shinikizo la kijamii, kwa kupunguza uwezo wa Hezbollah kuvutia wanachama wapya Kusini mwa Lebanon na Bekaa,

  • shinikizo la kijeshi, kwa kulenga ngazi za uongozi na uzalishaji wa ndani wa ndege zisizo na rubani na makombora.

Katika muktadha huo, vitisho vya mara kwa mara vya Marekani na Israel vinavyotumia misemo kama “tarehe ya mwisho” na “onyo la mwisho” ni jitihada za wazi za kulazimisha Lebanon kwenye mkondo wa shinikizo: ama kuvuliwa silaha kwa Hezbollah, au kubeba lawama ya kuanzishwa kwa vita vipya.

Ujumbe huu pia unaelekezwa kwa jamii ya ndani ya Israel, ili kuonyesha kuwa taasisi za usalama haziko tayari tena kupuuza hatari ya “kuongezeka kimyakimya kwa uwezo wa Hezbollah”.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha